Katika tukio la ziara yake rasmi ya kwanza nchini Marekani katika kipindi cha miaka saba, Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman atapokelewa na Donald Trump katika Ikulu ya White House siku ya Jumanne, Novemba 18.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ingawa viongozi hao wawili wanatarajiwa kutumia fursa hiyo tena kuonyesha uhusiano wao wa karibu, mkutano huo unaweza pia kuwa nafasi ya kulinganisha maono yao kwa Mashariki ya Kati. Kwa Saudi Arabia, ni azimio tu la swali la Palestina linaloweza kufungua njia ya kuhalalisha uhusiano na Israel.

Mkataba wa ulinzi wa Marekani na Saudi Arabia na mpango wa nyuklia wa kiraia unaoungwa mkono na Washington: hivi ndivyo Mohammed bin Salman, mtawala halisi wa ufalme wa Saudi Arabia, anatarajia kufanikisha wakati wa ziara yake nchini Marekani. Hii ni ziara ya kwanza ya Mwanamfalme wa Saudi Arabia huko Washington tangu mwaka 2018, mwaka wa mauaji ya mwandishi wa habari mkosoaji mkuba wa utawala wa kifalme wa Saudia, Jamal Khashoggi. Lakini jinsi siku hizo zinavyoonekana kuwa mbali wakati kifo cha kikatili cha msomi huyo wa Saudi Arabia, ambaye alikosoa waziwazi utawala wa Riyadh, kilimfanya Mohammed bin Salman kuwa mtu mwenye msimamo wa kutiliwa shaka.

Saudi Arabia inaona Israel kama “nchi inayodhoofisha ukanda mzima” wa Mashariki ya Kati.

“MBS,” kama anavyopewa jina la utani, amekuwa tena mmoja wa washirika muhimu wa Magharibi. Muhimu, haswa, katika Mashariki ya Kati iliyotumbukia katika machafuko tangu Oktoba 7, 2023, na shambulio la kigaidi la Hamas nchini Israel lililosababisha vita vya umwagaji damu huko Gaza. Kwa hivyo, ni pamoja na Saudi Arabia ambapo Ufaransa imejenga mpango wake mwaka huu unaolenga kufufua suluhisho la mataifa mawili. Na pia ni pamoja na Saudi Arabia ambapo Donald Trump anaota kukamilisha Makubaliano ya Abraham, ambayo, mnamo mwaka 2020, yalishuhudia Falme za Kiarabu, Bahrain, na Morocco zikirekebisha uhusiano wao na Israel.

Kwa muda mrefu, Riyadh iliweka “njia iliyo wazi ya taifa la Palestina” sharti la kuzingatia kuhalalisha na Israel. Sasa, ufalme huo unaondoa uwezekano wowote wa kurejesha uhusiano na Israeli ikiwa taifa hilo litaendelea kuzuia kuundwa kwa taifa huru la Palestina. “Saudi Arabia inapoitazama Israel leo, haioni tu vita huko Gaza na uvamizi wa Ukingo wa Magharibi; pia inaona kuhatarishwa kwa usalama kwa eneo lote,” anabainisha mtafiti, raia wa Ufaransa, Xavier Guignard, ambaye kwa sasa amealikwa katika Taasisi ya Mafunzo ya Kidiplomasia(Prince Saud al Faisal Institute for Diplomatic Studies).

“Sidhani kama Donald Trump kwa sasa yuko katika nafasi ya kulazimisha MBS kurudi nyuma katika suala la kurekebisha uhusiano wa Saudia na Israeli,” mtaalamu huyo ameiambia RFI katika mji mkuu wa Saudi Arabia. Sio lazima, kulingana na Xavier Guignard, kwa sababu “MBS hataki kumpa (Benjamin) Netanyahu ushindi wa kiiishara: anatumai kumuona akipoteza uchaguzi wa mwaka 2026 nchini Israel.”

Kutokubaliana pia kuhusu Iran

Kuhusu jukumu la Iran kikanda, Donald Trump na Mohammed bin Salman pia wana mitazamo tofauti. Jamhuri ya Kiislamu imepitia vikwazo vingi katika miezi ya hivi karibuni: ikiwa imeshambuliwa kwa mabomu na Israel na Marekani, pia imeathiriwa na kuanguka kwa utawala wa Syria wa Bashar Al Assad na kudhoofika kwa Hezbollah ya Lebanon, iliyoshindwa kijeshi kwa mashambulizi ya mabomu ya Israeli.

Kulingana na Xavier Guignard, Mwanamfalme wa Saudi Arabia anawasili Washington na pendekezo la kupatanisha kati ya Iran na Marekani. Tehran na Riyadh zimeanza uhusiano wa karibu katika miaka ya hivi karibuni, baada ya kipindi cha uhasama wa moja kwa moja. Sasa, “Saudi Arabia inataka kudhoofika kwa Iran kwa gharama yoyote ile,” mtafiti anaeleza. Mtazamo huu unapingana kabisa na ule wa mshirika mwingine mkuu wa Marekani katika eneo hilo, kwani Israel haitakuwa na chuki na kuanguka kabisa kwa Jamhuri ya Kiislamu.

Kuhusu suala la Syria, Donald Trump anaweza pia kulazimika kufikiria washirika wake wa Saudi Arabia na Israel. Kulingana na Xavier Guignard, “Saudi Arabia inawekeza kwa kiasi kikubwa, bila kizuizi, katika kujaribu kujenga upya Syria,” ambayo sasa inatawaliwa na Waislam kutoka dhehebu la Kisuni baada ya kuanguka kwa Bashar Al Assad. Kipaumbele cha Saudia kilichoathiriwa kwa kiasi kikubwa na mashambulizi ya Israel katika eneo la Syria yaliyotokea mwaka uliopita.

Je, masuala haya yatatoa kivuli juu ya uelewa ambao Mohammed bin Salman na Donald Trump wangependa kukisia? Mwaka huu, Saudi Arabia ilimkaribisha rais wa Marekani kwa ukarimu, ambaye alipokelewa katika ufalme huo katika majira ya kuchipua kwa ahadi ya uwekezaji wa dola bilioni 600 nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *