Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch linawatuhumu wanajeshi wa Mali na wanamgambo washirika kuua raia 31 na kuchoma moto nyumba zao katika mashambulio mawili tofauti kwenye vijiji kadhaa vilivyoko eneo la Segou mwezi uliopita.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Human Rights Watch inasema shambulio la kwanza lilitokea Oktoba 2 katika kijiji cha Kamona, ambapo jeshi na vikosi vya wanamgambo viliua watu wasiopungua 21 na kuchoma nyumba. La pili, iliripotiwa katika kijiji cha Balle karibu kilomita 55 (maili 34) kutoka eneo ambapo watu wasiopungua 10 akiwemo mwanamke mmoja walikuwa wameuawa.
Mashahidi wameiambia HRW kwamba wanajeshi na washirika wao waliwanyonga wakaazi, wakiwashutumu kwa kushirikiana na kundi la Jama’at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM), ambalo lina uhusiano na Al-Qaeda na linapanua kikamilifu operesheni zake kusini mwa nchi.

Wasemaji wa jeshi la Mali au Umoja wa Afrika hawajazungumzia lolote kuhusu madai haya.
Human Rights Watch ilitoa wito kwa mamlaka ya Mali kuchunguza mara moja mauaji hayo na kuutaka Umoja wa Afrika kuchukua hatua ili kusaidia kumaliza mzozo huo na kuwawajibisha wale waliohusika na uhalifu huo.
Mali, nchi isiyo na bandari, iko chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa vikundi vya kijihadi, ambavyo sio tu vinashambulia vikosi vya serikali lakini pia hivi karibuni viliweka kizuizi cha mafuta, na hivyo kuzidisha mzozo wa kiuchumi na kibinadamu katika eneo hilo.