Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limethibitisha kuwa, waasi wa AFC/M23, wanadhibiti mji wa Katoyi, wakati huu vita vikiendelea licha ya pande hizo mbili kukubaliana kuhusu namna ya kupata mkataba wa kudumu wa kusitisha mapigano.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mji huo wa Katoyi, ulio umbali wa Kilomita 100 kutoka Goma, ulichukuliwa na waasi hao baada ya mapigano makali siku ya Jumanne kati ya AFC/M23 dhidi ya jeshi, lililokuwa linashirikiana na wapiganaji Wazalendo.

Jeshi la DRC, limewashtumu waasi hao kwa kuendelea kuvunja makubaliano ya kusitisha vita, licha ya pande hizo mbili kutia saini maelewano mengine Jumamosi iliyopita nchini Qatar.

Soma piaM23 na serikali ya DRC walitia saini makubaliano ya amani

Viongozi wa eneo la Katoyi, wanasema mapigano hayo yamekuwa na madhara makubwa ambapo idadi kubwa ya watu wameyakimbia makaazi yao.

Hii inakuja baada ya waasi hao pia kuchukua maeneo ya Kazinga, Kasheke, na  Bibatama na sasa wanajaribu kufika mji wa Ntogo, Kilomita 40 kutoka kambi kubwa ya jeshi la DRC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *