Watalaam wa Umoja wa Mataifa kuhusu DRC, katika  utafiti wao wa hivi punde unaonesha malengo ya kisiasa ya Kundi la waasi la M23/AFC, ambalo  linahusishwa pia rais wa zamani Joseph Kabila ambaye anaongoza mchakato wa kundi hilo kubadilishwa likiwemo jina.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa uchunguzi wa watalaam hao, waasi wa AFC/M23  wana wapiganaji wapatao 30,000.

Wapiganaji hao wanajumuisha waliokuwa wapiganaji wa CNDP, Kundi la kwanza la M23 mwaka 2012, na tangu mwaka 2021 kundi hilo limekuwa likiwasajili wakimbizi kutoka Rwanda.

Aidha, maelfu ya waliokuwa wanajeshi wa serikali ya DRC, polisi na wapiganaji wa Wazalendo, walikamatwa na kulazimishwa kuungana na Kundi hilo la waasi, huku wengine wakiamua kujiunga kwa hiari.

Kuhusu malengo yao ya kisiasa, wataalam hao wa Umoja wa Mataifa, wamebaini kuwa Kundi hilo linataka kuundwa kwa Jamhuri ya Shirikisho la DRC, ambapo wapiganaji wake watakuwa wanajeshi wa nchi.

Pamoja na hili, waasi hao wanataka kuundwa kwa ukanda wa Mashariki ambao utajitegemea.

Ripoti ya wataalam hao pia imebaini kuwa rais wa zamani Joseph Kabila, amekuwa akitembelea maeneo yanayodhibitiwa na waasi hao tangu Mei mwaka 2025 na kukutana na viongozi wa Kundi hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *