Ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO, inasema kuwa, mwanamke mmoja kati ya watatu – ambao ni sawa na milioni 840 duniani kote, wamepitia ukatili wa kijinsia au unyanyasaji wa kimapenzi katika maisha yao.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti hiyo, wanawake na wasichana wenye umri kati ya miaka 15 na zaidi walipigwa na wapenzi wao au kudhulumiwa kimapenzi mwaka uliopita, ambapo wale wanaoishi katika nchi zinazokabiliwa na vita wakiwa kwa hatari kubwa.

WHO imesema kwenye ripoti yake kuwa, visa vya dhuluma dhidi ya wanawake vinasalia kupuuzwa dunaini kote, ikitaka hatua za dharura kuchukuliwa ikiwemo ufadhili kuongezwa kusaidia katika kampeni za kuzuia ukatili wa kijinsia.

Kwa mujibu wa WHO, ni asililia 0.2 pekee ya ufadhili ambayo ilielekezwa katika programu za kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake mwaka wa 2022, hofu ikiongezeka kuwa huenda visa vya dhuluma dhidi ya wanawake na wasichana vikaongeza baada ya Marekani kukatisha misaada ya kigeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *