
Ni takriban saa 48 zimesalia kwa wajumbe wanaoshiriki majadiliano katika mkutano wa tabianchi wa COP30, kuwa na rasimu ya makubaliano kufikia hapo kesho.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Siku ya Jumanne, rasimu ya kwanza ya maandishi ilipendekezwa na Brazil ambayo inashikilia urais wa mkutano huo, ambapo masuala manne muhimu yenye utata yalimulikwa likiwemo suala la upatikanaji wa fedha na matumizi ya mafuta ya kisukuku.
Wajumbe kutoka nchi zinazoendelea na wadau wengine wa mazingira wameendela kushinikiza fedha zaidi kwa ajii ya kugharamia mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Obed Koringo ni mtaalam wa sera kuhusu tabianchi kutoka shirika la Care International.
“Kwa muda mrefu mambo ya adaptation hayajapewa umuhimu unaostahili kutokana vikwazo vingi tu.” Alisema Obed Koringo ni mtaalam wa sera kuhusu tabianchi kutoka shirika la Care International.
Aidha katika majadiliano haya, Kudakwashe Majonjo kutoka shirika la Powershift Africa, anasema lazima dunia izingatie suala la nishati jadidifu na kuendeleza mabadiliko ya haki kuelekea uchumi safi zaidi.
“Kuhusu kuachana na mafuta ya kisukuku, kama Waafrika tumekuwa tukisema tulishinda vita hivi kule COP28 Dubai, na tukasema kutakuwa na mipango ya kuzidisha mara tatu matumizi ya nishati jadidifu. ikiwa yatakayoafikiwa yatakwenda zaidi ya COP28, hicho ndicho cha maana.” Alisema Kudakwashe Majonjo kutoka shirika la Powershift Africa.
Rukiya Khamis kutoka shirika la 350.org anasema, anasma makubaliano ya COP30 yatakuwa dhaifu ikiwa mambo haya hayatajumuishwa.
“Kuhusu kuachana na mafuta ya kisukuku kama Waafrika tumekuwa tukisema tumeshinda vita hii kule COP28 Dubai na tukasema kutakuwa na mipango ya kuzidisha mara tatu mipango ya nishati jadidifu.” Alisema Rukiya Khamis kutoka shirika la 350.org
Rasimu nyingine ya maandishi inatarajiwa kutolewa asubuhi ya Alhamisi tarehe 20.
Ripoti ya Minzilet Ijai imesomwa naye Hillary Ingati.