Mabalozi wa nchi 15 wanachama wanatarajiwa kuzuru Damascus Disemba 4, siku chache kabla ya kumbukumbu ya kwanza tangu kuondolewa madarakani kwa mtawala wa muda mrefu wa Syria Bashar al-Assad.

Wanadiplomasia hao wanatarajiwa kukutana na mamlaka mpya ya Syria, hususan Rais Ahmed al-Sharaa, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kujiimarisha upya nchini humo.

Baraza hilo hivi karibuni lilimuondolea vikwazo al-Sharaa mpiganaji wa zamani wa jihadi, likimtolea wito wa kuwa na kipindi cha mpito jumuishi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *