
Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza yameua watu wasiopungua sita siku ya Jumapili, Juni 14, kulingana na maafisa wa uokoaji na vyanzo vya hospitali katika eneo la Palestina, licha ya mapigano yanayoendelea.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shambulio la anga la Israel kwenye kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa eneo hilo limeua watu wanne na kuwajeruhi wengine kadhaa, limeripoti Shirika la Ulinzi la Raia, shirika la huduma ya kwanza linalofanya kazi chini ya mamlaka ya harakati ya Kiislamu Hamas.
Hospitali ya Al-Shifa katika Jiji la Gaza imeripoti kupokea miili minne kufuatia shambulio hilo na kuwatibu watu watano waliojeruhiwa. Msemaji wa jeshi la Israel ameliambia shirika la habari la AFP kwamba shambulio la Jabalia lililenga “magaidi wa Hamas.” Watu wengine wawili walmeawa na risasi za Israel katika matukio tofauti katika eneo la Khan Younis (kusini), kulingana na Shirika la Ulinzi la Raia.
Ukanda wa Gaza ambao bado uko chini ya vikwazo vikali vya Israel kuhusu misaada ya kibinadamu, umeharibiwa na vita vya zaidi ya miaka miwili, vilivyosababishwa na shambulio lisilo la kawaida la Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7, 2023.
Angalau Wapalestina 986 wameuawa tangu kutangazwa kwa usitishaji mapigano, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo, ambayo iko chini ya udhibiti wa Hamas na ambayo takwimu zake zinachukuliwa kuwa za kuaminika na Umoja wa Mataifa. Jeshi la Israel limeripoti vifo vitano miongoni mwa safu zake katika kipindi hicho.