Marekani. Mwigizaji  na mwanamitindo wa Kenya, Lupita Nyong’o amesema filamu ya 12 Years a Slave, imempa madili mengi ikiwamo kucheza nafasi kama aliyocheza.

Katika filamu hiyo, Lupita alicheza nafasi ya Patsey, mwanamke mweusi aliyekuwa mtumwa anayebaguliwa.

Katika mahojiano na CNN inside Africa, muigizaji huyo alisema baada ya filamu hiyo kutoka mwaka 2013 matarajio yake ilikuwa apewe nafasi tofauti tofauti lakini hali haikuwa kama alivyotarajia.

“Ilinipa mwongozo wa kila kitu nilichofanya tangu wakati huo. Lakini kinachofurahisha ni baada ya kushinda tuzo ya Academy, ungetegemea, ‘Ah, sasa nitapata nafasi kuu hapa na pale.’”

“Badala yake ilikuwa, ‘Lupita, tungependa ucheze filamu nyingine na wewe ni mtumwa, lakini safari hii uko kwenye meli ya watumwa.’ Hizo ndizo nafasi nilizokuwa nikipata miezi michache baada ya kushinda Oscar.”

“Hata vyombo vya habari Marekani viliandika mengi mara huu utakuwa mwisho wa Lupita lakini nililazimika kujifunga masikio dhidi ya wapiga ramli hao kwa sababu, mwishowe mimi si nadharia mimi ni mtu halisi na ni Mwafrika kweli.”

Kwa sasa, Lupita anatarajiwa kuigiza katika filamu ijayo ya Lunik Heist.

Miongoni mwa tuzo alizowahi kuchukua Lupita ni Oscar (Academy Award kama Best Supporting Actress katika filamu ya 12 Years a Slave. Screen Actors Guild (SAG) Award kama Best Supporting Actress katika filamu hiyo hiyo.

Independent Spirit Award na New York Film Critics Online Award kama Best Actress kwa US.

Pia aliwahi kutokea kama video vixen kwenye ngoma za wasanii maarufu kama Beyonce kwenye wimbo wa Brown Skin Girl aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria, Wizkid. Jay Z kwenye wimbo wa MaNyfaCedGod na nyinginezo.

Lupita ni mtoto wa Profesa Anyang Nyong’o na mwanasiasa mashuhuri na msomi Kenya. Aliwahi kuwa Seneta wa Kaunti ya Kisumu na Waziri wa Afya na Waziri wa Mipango.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *