Marekani. King Comb, mtoto wa kiume wa Rapa na Mfanyabiashara maarufu duniani, Sean ‘Diddy’ Combs amesema anaamini baba yake anaweza kuachiwa mapema kutoka gerezani kabla ya msimu wa Krismasi.

P Diddy, mwenye umri wa miaka 56 anatumikia kifungo cha miezi 50 jela baada ya kupatikana na hatia kwa makosa mawili ya kusafirisha watu kwa ajili ya uasherati. Iliripotiwa awali anatarajiwa kuachiwa Juni 4, 2028

Hata hivyo, King mwenye umri wa miaka 27 anaamini baba yake atarejea nyumbani hivi karibuni.

King aliambia TMZ.com: “Atakuwa njiani kurudi nyumbani. Anaendelea vizuri, kila kitu kiko sawa. Atakuwa nyumbani hivi karibuni.”

Alipoulizwa huenda nguli huyo wa hip-hop akapata msamaha wa serikali ya Marekani, King alijibu: “Tutaona. Tuombee tu.”

King pia aliulizwa jinsi familia inavyojiandaa kwa msimu wa likizo bila uwepo wa P Diddy na amesema; “Angalieni tu huenda akarudi nyumbani kabla ya hapo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *