Kampuni ya Strategis Insurance imewahimiza wamiliki wa shule nchi nzima kuhakikisha kwamba wanayakatia bima kubwa mabasi yao ya kubebea wanafunzi.
Licha ya jukumu muhimu la mabasi hayo katika usalama wa wanafunzi na shughuli za shule, shule nyingi zimeendelea kutumia bima ndogo na hivyo kujiweka katika hatari kubwa ya hasara za kifedha pamoja na kuharibu sifa za shule zao.
Mabasi ya shule ni zaidi ya magari; ni mali muhimu zinazohakikisha usafiri salama wa wanafunzi, wafanyakazi, na vifaa vingine. Hata hivyo, shule nyingi huchagua malipo kidogo ya bima, mara nyingi kutokana na vikwazo vya bajeti au ukosefu wa ufahamu kuhusu hatari wanazoweza kukutana nazo kutokana na kukosa bima kubwa. Hii inaweza kusababisha shule kuingia gharama kubwa kutokana na tukio la ajali, wizi, au matukio mengine yasiyotarajiwa.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategis Insurance (Kitengo cha Bima za Mali na Ajali), Jabir Kigoda
Akizungumzia dhamira ya kampuni hiyo katika kutoa huduma bora za bima kwa taasisi za elimu, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategis Insurance (Kitengo cha Bima za Mali na Ajali), Jabir Kigoda anasema:
“Strategis Insurance tunatambua changamoto zinazokabili shule katika kulinda mali zao. Bima zetu kubwa zimeundwa ili kuwapa wamiliki wa shule utulivu wa akili, kuhakikisha kwamba shule zinaendelea kutoa huduma na kutekeleza malengo yake ya msingi ya kutoa elimu pasipo kufikiria changamoto za kifedha zinazoweza kutokea.”
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu (Group CEO), Dk Flora Minja alisisitiza umuhimu wa kukinga mali ambapo anasema: “Kuwekeza katika bima kubwa sio tu uamuzi wa sahihi wa kifedha bali ni hatua muhimu kuelekea usalama na ustawi wa wanafunzi na wafanyakazi.”
Anaongeza kuwa kwa kushirikiana na Strategis Insurance, shule zinaweza kuhakikisha kuwa zinakuwa na kinga dhidi ya hatari zinazohusiana na usafiri wa shule.
Strategis Insurance inawahimiza wamiliki wote wa shule kutathmini upya sera zao za sasa za bima na kuzingatia bima kubwa ambayo inatoa kinga dhidi ya hatari zote zinazoweza kutokea kwenye mabasi ya shule. Kwa kufanya hivyo, shule zinaweza kulinda mali, wanafunzi, wadau na kujijengea sifa kama taasisi zilizojidhatiti kufanya vyema katika sekta ya elimu, anaeleza zaidi.
Strategis Insurance imebobea katika utoaji wa bima za muda mfupi, yaani bima za mali na ajali, Bima za afya. Huduma zetu ni pamoja na bima za watu binafsi na za kibiashara kama vile Bima za Magari, Moto, Wizi, Kilimo, Usafiri, Trekta na Bima ya Kontena.
Huduma za bima kutoka Strategis Insurance zinapatikana Tanzania nzima kupitia vituo vya mauzo vya Dar es Salaam (City Centre), Mbeya, Mwanza, Dodoma, Arusha na Zanzibar, kampuni hiyo imejipanga vyema kuhudumia shule, mashirika na watu binafsi nchi nzima.