Mkurugenzi wa baraza la wakimbizi la Uholanzi, amesema nchi zinazoendelea ambazo nyingi zinatoa hifadhi kwa wakimbizi, huenda zikafunga mipaka yao ikiwa mataifa ya magharibi yataendelea kupunguza misaada yao.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakati huu mataifa kama Uingereza na Ujerumani yakichukua hatua kali kudhibiti wimbi la wahamiaji na waomba hifadhi, mataifa mengine nayo yameendelea kupunguza misaada yao kwa mamilioni ya raia ambao wamekimbia machafuko kwenye nchi zao.

Charlotte Slente, katibu mkuu wa baraza hilo, amesema wanaguswa na mataifa yanayoendelea ambayo yanachukua asilimia zaidi ya 70 ya wakimbizi, kwamba nchi hizo nazo zitalazimika kuchukua hatua kudhibiti wakimbizi kuingia kwenye mataifa yao.

Wakimbizi wa Sudan wakiwa kwenye foleni ya kujaza maji katika kambi ya Oure Cassoni nchini Chad Novemba 12, 2025. (Picha: Joris Bolomey / AFP)
Wakimbizi wa Sudan wakiwa kwenye foleni ya kujaza maji katika kambi ya Oure Cassoni nchini Chad Novemba 12, 2025. (Picha: Joris Bolomey / AFP) AFP – JORIS BOLOMEY

Shirika hilo lilitolea mfano nchi za Uganda, Chad na Cmaeroon ambazo kwa miaka zimeonesha ukarimu kwa kuwapokea wakimbizi kutoka Sudan, Sudan Kusini na Somalia, sasa zimeanza kudhibiti idadi ya wakimbizi inaowapokea.

Aidha baraza hilo linasema uamuzi wa Marekani kusitisha misaada ya nje kumeathiri pakubwa shughuli za mashirika ya misaada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *