#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya, Mh. Patrick Mwalunenge ameendelea kutekeleza ahadi zake za kuwawezesha wananchi kiuchumi baada ya kukabidhi pikipiki saba kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Hatua hii imekuja mara tu baada ya kurejea kutoka Bungeni jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kuongeza mazingira rafiki ya ajira na kukuza uchumi wa vijana, sambamba na kupunguza utegemezi na changamoto za ajira mijini.
Pikipiki hizo zimegawiwa kwa vijana kutoka maeneo ya Nzovwe (1), Kiwira (4), Mwanjelwa (1), na Uyole (1), huku zaidi ya vijana 300 wa bodaboda wakiwezeshwa mafuta kama sehemu ya kuwapa nguvu ya kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Mbunge Mwalunenge amesisitiza kuwa kazi ya bodaboda ni sekta halisi ya uchumi inayogusa maisha ya watu wengi, hivyo vijana wanapaswa kuiheshimu, kuithamini na kuifanya kwa weledi, kwani kupitia uaminifu na bidii wanaweza kujijenga na kubadilisha maisha yao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania