#HABARI: Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Mhe. Christine Grau walipomtembelea leo Desemba 4, 2025 katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, walizungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha diplomasia ya kibunge (Parliamentary Diplomacy).
Kikao hicho kimehudhuria na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania ambao ni Balozi wa Finland, Balozi wa Hispania, Balozi wa Italia, Balozi wa Ubelgiji na Balozi wa Ujerumani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania