#HABARI: Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeibuka mshindi wa kwanza na kupewa tuzo ya umahiri katika utayarishaji bora wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2024 kwa kufuata viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu International Public Sectors Accounting Standards (IPSAS) katika kundi la Taasisi za Serikali zinazojitegemea.
Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA APC hotel Bunju jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amekipongeza Kitengo cha Fedha na Uhasibu kwa kufanikisha uandaaji bora wa hesabu uliopelekea kuwa washindi wa tuzo hiyo.
“Niwashukuru watumishi wote wa Mamlaka hasa timu ya fedha na ukaguzi wa ndani kwa kujitoa, kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha kuwa taarifa zetu za fedha zinaandaliwa kwa kiwango cha juu kinachotambulika kimataifa. Tuzo hii ni matokeo ya kazi yao nidhamu, na ushirikiano ndani ya Taasisi,” amesema Kamishna Jenerali Lyimo.
Kamishna Lyimo ameongeza kuwa, ushindi wa tuzo hii ni ushahidi kwamba Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inafuata na kuzingatia Sheria za Fedha, Manunuzi na miongozi mbalimbali fedha inayotolewa na Hazina kwa nyakati mbalimbali.
Hii ni mara ya nane DCEA kushinda tuzo hizi tangu mwaka 2017 na itaendelea kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha kuwa inatimiza majukumu yake kwa ufanisi na kwa manufaa ya watanzania wote.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania