Idadi ya vifo kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyoambatana na Kimbunga Ditwah nchini Sri Lanka wiki iliyopita imeongezeka hadi 607, Kituo cha Usimamizi wa Maafa (DMC) kimetangaza leo Ijumaa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watu milioni 2 wameathiriwa na janga hili la asili, ambalo ni janga kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini humo tangu Tsunami ya mwaka 2004, na watu 214 bado walikuwa hawajulikani walipo kufikia Ijumaa, DMC imeongeza.

Shirika la kitaifa linalohusika na Usalama wa Majengo (NBRO), ambalo dhamira yake ni kufuatilia utulivu wa ardhi, limetoa maonyo mapya ya hali mbaya ya hewa leo Ijumaa kwa sehemu ya kati ya kisiwa hicho, ambacho kina watu milioni 22.

“Mvua ilizidi milimita 150 katika baadhi ya maeneo katika saa 24 zilizopita. Ikiwa itaendelea, jikingeni ili kuepuka hatari ya maporomoko ya ardhi,” NBRO imeonya. Maji ya mafuriko yaliyofurika vitongoji vingi vya mji mkuu, Colombo, yameendelea kupungua, na kuwezesha baadhi ya wakazi kurudi majumbani mwao.

Usafi na tathmini wa uharibifu

Idadi ya watu waliohamishwa na janga hilo na kuwekwa katika makazi ya dharura imepungua kutoka 225,000 hadi 170,000. Katika majimbo ya kati, shughuli za usafi zimeendelea Ijumaa, haswa kwa msaada wa jeshi, ambalo limepeleka maelfu ya wanajeshi katika maeneo yaliyokumwa na mafuriko na yaliyoharibiwa.

Kulingana na kamishna wa huduma muhimu wa serikali, umeme umerejeshwa karibu robo tatu ya nchi, huku baadhi tu ya maeneo katika eneo la kati yakiwa bado hayana umeme na huduma ya simu. Mamlaka imekadiria gharama ya kujenga upya nchi, ambayo uchumi wake unatoka tu kutoka kwenye mgogoro mbaya zaidi katika historia yake mwaka 2022, kuwa kati ya dola bilioni 6 na 7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *