Mwenyekiti wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ameandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii kwamba: “Ukiukaji wowote wa ahadi utakaofanywa na Marekani au kujiondoa katika fremu kuu ya maelewano kutapelekea jeshi la Iran, kwa uungaji mkono wa taifa shupavu la Iran kutoa jibu kali, thabiti na la kuumiza zaidi dhidi ya adui huyo kuliko ilivyokuwa huko nyuma.”

Ebrahim Azizi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, ameandika katika ukurasa wake binafsi katika mtandao wa X kwamba: “Muqawama wa kijasiri wa wananchi wa Iran umeipelekea Marekani kutokuwa na budi ila kuketi kwenye meza ya mazungumzo na kukubali masharti ya Iran. Sasa Marekani ina wajibu wa kuvutia imani ya wananchi wa Iran kwa kutekeleza vipengee vyote vya mkataba wa maelewano, ikiwa ni pamoja na kusimamisha vita dhidi ya Lebanon na kuondolewa haraka utawala bandia wa Israel katika eneo la kusini mwa Lebanon.

Amesisitiza kuwa: Ukiukaji wowote wa ahadi au kuondoka katika fremu kuu ya maelewano kutapelekea jeshi la taifa shujaa la Iran kujibu na kutoa jibu kali na la nguvu kubwa zaidi kuliko huko nyuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *