
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer atakuwa mwenyeji wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini London baadaye hii leo, wakati huu Kyiv ikitafakari hatua zinazofuata baada ya mazungumzo ya amani ya Marekani kuhusu kumaliza vita na Urusi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mazungumzo hayo kati ya Starmer na Zelensky Jumatatu hii, yataangazia pakubwa pendekezo la Marekani la kumaliza uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Viongozi wengine ambao watahudhuria mkutano huo ni rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na kansela wa Ujerumani Friedrich Merz.
Ikulu ya White House imekuwa ikishinikiza Kyiv na Moscow kukubaliana na mpango wa kumaliza vita lakini kumekuwa na dalili ndogo ya mafanikio.
Mazungumzo yanabaki kukwama katika masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na ukubwa wa jeshi la Ukraine baada ya vita kumalizika, na udhibiti wa Urusi wa eneo la Donbas.