#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linafanya uchunguzi wa tukio la ajali ya gari kuwaka moto na kuteketea.

Tukio hilo limetokea Decemba 9, 2025 asubuhi eneo la Maseyu kona kali, kata ya Gwata, wilaya ya Morogoro, gari lenye namba za usajili T. 947 DVR
aina ya TATA likisafiri kutoka Dar es salaam kwenda wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro, likiendeshwa na Halfan Omary, dereva na mkazi waMbezi Dar es salaam, likiwa na abiria 40 liliwaka moto na kuteketea.Katika tukio hilo hakuna abiria aliyepata madhara.

Hata hivyo, mizigo na mali zingine za abiria ndani ya basi hilo zimeharibika na kuteketea. Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya mifumo ya
umeme wa gari hilo. Uchunguzi zaidi unaendelea

Jeshi la Polisi linawakumbusha wamiliki wa vyombo vya moto kuwa na utamaduni wa kufanya matengenezo ya mara kwa mara wa magari yao hasa yanayobeba abiria ili kuokoa maisha ya watu na mali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *