
Shirikisho la Nchi za Sahel barani Afrika linalojumuisha Mali, Niger na Burkina Faso (AES) limetangaza kuwa litazizuia ndege zote zinazokiuka anga yashirikisho hilo kufuatia ripoti za ukiukaji wa sheria uliofanywa na Nigeria.
Shirikisho la Nchi za Sahel (AES) limeeleza kuwa ndege ya Jeshi la Anga la Nigeria C-130 ilitua kwa dharura nchini Burkina Faso, na kwamba uchunguzi wa mamlaka ya Burkina Faso umebaini kuwa ndege hiyo ilitua bila ya kibali.
Shirikisho la Sahel limelaani kukikwa anga yake kulikofanywa na ndege ya Jeshi la Anga la Nigeria na kusisitiza kuwa maafisa husika wa shirikisho hilo wamepewa mamlaka ya kuziozuia ndege zote zitakazokiukaanga ya shirikisho hilo la Sahel.
Muungano wa nchi za Sahel umeutaja ukiukaji huo uliofanywa na ndege ya Nigeria kuwa hatua isiyo ya kirafiki bila kujali sheria za kimataifa na kanuni za kimataifa za kiraia na kijeshi.
Mali, Burkina Faso, na Niger nchi zinazopitia matatizo yanayofanana zilianzisha Shirikisho la Nchi za Sahel Julai 6 mwaka jana kufuatia kupitishwa kwa Mkataba wa Liptako-Gourma, ambao uliasisi Muungano wa Nchi za Sahel Septemba 16, 2023.
Shirikisho hilo limechukua hatua za kijasiri kutathmini upya muungano wake wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na kujiondoa hivi karibuni kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) na Shirika la Kimataifa la La Nchi Zinazozungumza Lugha ya Kifaransa (OIF).