Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama amefariki dunia leo Desemba 11, 2025 jijini Dodoma.
“Kwa masikitiko makubwa, natangaza kifo cha Mbunge wa Perahimo, Jenista Mhagama kilichotokea leo 11 Desemba, 2025 jijini Dodoma. Natoa pole kwa waheshimiwa wabunge wote, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Peramiho,” amesema Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu katika taarifa ya Bunge kwa umma.
Kwa mujibu wa ofisi ya Bunge, mipango ya mazishi na taarifa Zaidi zitaendelea kutolewa.
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)