Mbunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, Jenista Mhagama amefariki Dunia leo jijini Dodoma.

Taarifa ya kifo chake imetolewa na Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ambaye ametoa pole kwa watu wote wanaohusika na msiba huo.

Amesema hivi sasa Bunge linashirikiana na familia ya marehemu Mhagama kuratibu mipango ya mazishi ambapo utaratibu utaendelea kutolewa.

Rais Samia Suluhu Hassan ameomboleza kifo hicho akisema kwa miaka 38 marehemu amekuwa mwanachama mahiri wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kiongozi wa vijana na wanawake pamoja na waziri katika awamu mbalimbali.

Marehemu Jenista Mhagama amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 58.

Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *