#HABARI: Maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Joakim Mhagama yanaarajiwa kufanyika Desemba 16, 2025, katika Kijiji cha Ruanda wilayani Mbinga, ambapo kabla ya maziko, Desemba 15 shughuli za kuaga zitaendelea Peramiho, Songea Vijijini, kupitia ibada itakayofanyika katika Kanisa Katoliki la Peramiho, kisha waombolezaji wa eneo hilo watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho.
Ratiba iliyotolewa na Bunge la Tanzania imeeleza kuwa maombolezo yameanza leo nyumbani kwake eneo la Itega jijini Dodoma kabla ya kesho Desemba 13 ibada ya kumuaga marehemu kufanyika katika Kanisa Katoliki Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma, ikihudhuriwa na waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali.
Baada ya ibada hiyo, mwili utasafirishwa kuelekea Songea ambapo Desemba 14, maombolezo yataendelea nyumbani kwa marehemu katika eneo la Makambi, Songea Mjini huku jioni ya siku hiyo, mwili ukitarajiwa kupelekwa katika Kanisa Katoliki Matogoro kwa ibada nyingine kabla ya kurejeshwa nyumbani.
Aidha, Maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Joakim Mhagama, yameanza leo Desemba 12 jijini Dodoma.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania