#HABARI: Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Salome Makamba, ameeleza kuwa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika kujenga kituo cha kujaza gesi asilia kwenye vyombo vya usafiri katika eneo la Mlimani jijini Dar es Salaam, ambapo zaidi ya Shilingi Bilioni 12, zimetumika kukamilisha kituo hicho chenye uwezo wa kuhudumia magari madogo na bajaji 800 kwa siku.

Mhe. Salome amebainisha hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kukagua kituo hicho kinachosimamiwa na Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) ya GASCO.

“Matumizi ya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) yamerahisisha gharama za maisha kwa watu wa vyombo vya usafiri kwani gharama ya gesi kilo moja ni shilingi 1500 ambapo ukiwa na mtungi wa Kilo 17 unaweza kusafiri umbali wa KM 50 hii inaonesha dhahiri kuwa gesi ina gharama nafuu zaidi kuliko mafuta lakini pia kutokana na wingi wa magari ya biashara na bajaji katika Mkoa wa Dar es Salaam uwekezaji huu umekuwa ni fursa kwa wafanyabiashara hao katika kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza kipato,” amesema Mhe. Salome.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetan

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *