HABARI: Viongozi mbalimbali wanaendelea kuwasili nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama kwa ajili ya kutoa salamu za pole kwa familia.

Hali ya huzuni imetanda nyumbani hapa huku maandalizi ya awali ya msiba yakiendelea kuratibiwa nyumbani kwa marehemu Itega jijini Dodoma.

Leo hii majira ya saa kumi na moja jioni mwili wa marehemu ufikishwa nyumbani kwake kwa ajili ya taratibu nyingine za ibada ya kumuaga itakayofanyika katika Kanisa Katoliki la Kiwanja cha Ndege.

Jenista Mhagama amefariki dunia jana, Desemba 11, 2025, jijini Dodoma na taarifa za kifo chake zilitolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azzan (Zungu).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *