Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kimesema siku ya Alhamisi, Desemba 11, kwamba zaidi ya watu 2,000 waliuawa katika vurugu za mwishoni mwa mwezi Oktoba na mwanzoni mwa mwezi Novemba, na kutoa wito wa vikwazo dhidi ya wale waliohusika, ambao kinawatuhumu kwa uhalifu dhidi ya binadamu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Samia Suluhu Hassan alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 29 kwa karibu 98% ya kura, lakini serikali yake inashutumiwa kwa uwizi wa kura na kupanga kampeni ya mauaji na utekaji nyara wa wakosoaji wake katika kuelekea uchaguzi, ambao ulisababisha maandamano ya kupinga serikali kote nchini.

Makamu wa rais wa chama cha upinzani cha Chadema, John Heche, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Tanzania imepitia “mauaji ya watu zaidi ya 2,000 na zaidi ya 5,000 kujeruhiwa katika kipindi cha wiki moja.” Alidai kwamba vitendo hivi vya vurugu vilifanywa “kwa ushiriki wa moja kwa moja wa Serikali” na kwamba ni “uhalifu dhidi ya binadamu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *