Wito huu umetokana na uchambuzi wa zaidi ya tafiti 6,500 za jenomiki zilizosajiliwa kati ya mwaka 1990 na 2024, huku ongezeko kubwa likionekana tangu 2010. 

Uchambuzi uliochapishwa na WHO unaonesha kwamba ongezeko hili linahusiana na maendeleo katika teknolojia za upandikizaji wa jenomu au genome, kupungua kwa gharama, na upanuzi wa matumizi ya kliniki ya mbinu hii.

media:entermedia_image:35554d70-02fd-42f2-b854-1668d303c44b

Jinsi Hondurus ilivyoweza kuweka mffumo wa vinasaba wakati wa janga la COVID-19 (2023)

Ujumuishaji wa utafiti 

Jenomiki ni tawi la jenetiki linalosoma vinasaba kamili vya kiumbe, ikiwa ni pamoja na upandikizaji na uchambuzi. Saratani na magonjwa nadra ndiyo yanayotumika zaidi kwenye utafiti huu, yakionesha ujumuishaji wa karibu wa jenomiki katika maeneo haya. 

Hata hivyo, utafiti wa WHO unaonesha kutokubaliana pale tunapoangalia ni wapi na kwa nani tafiti hizi zinafanywa. Zaidi ya asilimia 80 ya tafiti za jenomiki za kliniki hufanyika katika nchi zenye kipato cha juu, huku chini ya asilimia 5 zikifanyika katika nchi zenye kipato cha chini na cha wastani. 

Kwa mujibu wa WHO mara nyingi, nchi hizi hushiriki tu kama maeneo ya pili ya utafiti, kutokana na uhaba wa uwezo wa upandikizaji wa jenomu na miundombinu ya utafiti.

media:entermedia_image:9243e08e-5f04-473d-99f7-ddb2f2c03c18

WHO/P. Phutpheng

Mtaalam wa maabara akifanya kazi katika kituo cha afya , sayansi na utafiti Bangkok

Mapengo na wasiwasi

WHO inaonesha kuwa mapengo makubwa ya kidemografia yamebainika. Zaidi ya asilimia 75 ya tafiti zinajumuisha watu wazima wenye umri kati ya miaka 18 na 64, huku asilimia 4.6 tu zikilenga watoto na asilimia 3.3 tu zikilenga watu wazee. Magonjwa yanayoweza kuambukiza, ambayo bado ni tatizo kubwa la afya ya umma katika maeneo mengi, hayana uwakilishi wa kutosha, yakichangia tu asilimia 3 ya tafiti zote za jenomiki za kliniki. 

Ripoti hiyo inasisitiza haja ya utafiti wa jenomiki unaojumuisha zaidi, wenye utofauti wa kijiografia, na unaoelewa muktadha wa kiasili.

Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi kwa Afya wa WHO, Meg Doherty, amesema shirika hilo litaunga mkono juhudi za kuhakikisha kuwa utafiti wa jenomiki unaakisi utofauti wa idadi ya watu duniani na mahitaji ya afya ya umma.

Kwakutumia utaalamu wa IAEA's wa kiufundi, kisayansi na uwezo wa maabara, ZODIAC wataanzisha mtandao ulimwenguni kote kusaidia maabara za kitaifa katika kufuatilia, na kugundua mapema pamoja na kudhibiti magonjwa kama Ebola na COVID-19

IAEA/Dean Calma

Kwakutumia utaalamu wa IAEA’s wa kiufundi, kisayansi na uwezo wa maabara, ZODIAC wataanzisha mtandao ulimwenguni kote kusaidia maabara za kitaifa katika kufuatilia, na kugundua mapema pamoja na kudhibiti magonjwa kama Ebola na COVID-19

Uwekezaji, watoto na wazee

Meg Doherty amesema kwamba kama kutokubaliana kwa ripoti hakutatatuliwa kimkakati, kunaweza kuongeza pengo la ukosefu wa usawa lililopo na kupunguza manufaa ya sayansi ya jenomiki kwa idadi ya watu ambao wangefaidika zaidi. 

WHO inapendekeza hatua kama vile kuongeza uwekezaji katika miundombinu ya jenomiki na uwezo wa utafiti katika maeneo yasiyowakilishiwa vizuri na kuhusisha zaidi watoto, wazee, na makundi mengine yasiyojumuishwa katika tafiti za kliniki.

Uchambuzi huu umezingatia matumizi ya jenomiki ya binadamu katika utafiti wa kliniki, ukijumuisha zaidi ya miongo mitatu ya tafiti zilizosajiliwa kati ya mwaka 1990 na 2024, na kutoa muhtasari mpana zaidi kuwahi kufanywa juu ya matumizi ya teknolojia hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *