#HABARI: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevunja rekodi kwa kukusanya Sh. Trilioni 4.13 kwa mwezi Disemba 2025 pekee, ikiwa ni ufanisi wa asilimia 102.9 ya lengo lililowekwa. Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda, amebainisha kuwa katika kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Disemba, mamlaka imekusanya jumla ya Sh. Trilioni 9.8, kiasi ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 12.26 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha uliopita.

Mafanikio haya ya makusanyo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uhimilivu wa shughuli za kiuchumi nchini uliopatikana chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na miongozo thabiti ya Serikali ya Awamu ya Sita. Kamishna Mwenda ameeleza kuwa wastani wa makusanyo kwa mwezi kwa nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/2026 umepanda hadi Sh. Trilioni 3.13, ikilinganishwa na wastani wa Sh. Trilioni 2.75 uliorekodiwa mwaka uliopita.

Ongezeko hili pia limetokana na kuboreshwa kwa mahusiano na walipakodi, kuimarisha matumizi ya mashine za EFD, na utatuzi wa migogoro ya kikodi kupitia majadiliano ya nje ya Mahakama ambapo makubaliano 42 yenye thamani ya Sh. Bilioni 9.4 yalifikiwa. TRA sasa inaelekeza nguvu zake katika kufikia lengo la mwaka la Sh. Trilioni 36.06, ikilenga kukuza mchango wa makusanyo ya kodi kwenye Pato la Taifa kufikia zaidi ya asilimia 14.1.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *