Wawakilishi wengine kutoka pembe ya Afrika katika michuano ya mwaka huu ya AFCON inayoendelea nchini Morocco, nchi ya Sudan wamefanikiwa kufuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo licha ya kupoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Burkina Faso.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Sudan waliokuwa Kundi E pamoja na Algeria, Burkina Faso na Equatorial Guinea, walipoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Burkina Faso kwa kufungwa magoli 2 kwa 0, taifa hilo likifunzu kama mshindi watatu bora kwenye Kundi lake.

Kwa upande wake Algeria ambayo tayari ilikuwa na tiketi mkononi hata kabla ya mechi ya jana, walimaliza vema hatua ya makundi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3 kwa 1 dhidi ya Equatorial Guinea iliyomaliza bila alama kwenye Kundi lake.

Mechi nyingine zilikuwa ni zile za Kundi E ambapo mabingwa watetezi Ivory Coast, walifanikiwa kuwa vinara kwenye Kundi hili baada ya kutoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 3 kwa 2 dhidi ya Gabon, huku Cameroon wao wakimaliza kwenye nafasi ya pili baada ya ushindi wa goli 2 kwa 1 dhidi ya Msumbiji.

Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo leo na kesho ni mapumziko, ambapo timu zilizofuzu hatua ya 16 bora ni pomoja na Sudan, Tanzania, DRC, Afrika Kusini, Senegal, Cameroon, Ivory Coast, wenyeji Morocco, Algeria, Burkina Faso, Misri, Benin, Nigeria, Msumbiji, Mali Pamoja na Tunisia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *