Muungano wa mashirika ya kiraia nchini Sudan, yameikosoa tume ya Umoja wa Afrika kwa kukaribisha mpango wa amani uliopendekezwa na Serikali ya kijeshi, ikitaja uamuzi huo kama wa hatari na unaenda kinyume juhudi za kikanda.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangazo la mashirika haya linakuja siku chache kupita tangu Kamishna wa Umoja Afrika, Mahmoud Ali Youssouf kusema kuwa ofisi yake inakaribisha mapendekezo ya Waziri Mkuu wa mpito wa Sudan, Kamil Idris aliyoyatoa kwenye baraza la usalama, akiyataja kama msingi kuelekea kupata amani.

Kufutia kauli yake, Waziri Mkuu wa zamani wa Sudan, Abdlah Hamdock anayeoongoza muungano wa SOMOUD, amekosoa msimamo wa AU, akisema umeonesha wazi kuwa na upendeleo akihoji iweje tume iunge mkono suluhu ya kijeshi kinyume na msingi wake unaopinga suluhu za kijeshi.

Mahmoud Ali Youssouf - Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika AUC.
Mahmoud Ali Youssouf – Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika AUC. AP – Frank Franklin II

Muungano huo ukiutuhumu umoja wa Afrika kwa kupuuza mpango wa amani uliokuwa umeratibiwa na nchi ya Qatar, ambapo ulitaka kuwepo kwa miezi mitatu ya usitishaji mapigano na kuruhusu misaada ya kibinadamu.

Mapendekezo ya utawala wa kijeshi yanajumuisha kuondoka kwa wapiganaji wa RSF kwenye maeneo wanayoyakalia na kuwepo kwa timu ya waangalizi wa AU, UN n anchi za kiarabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *