Wananchi wa Marekani wamemiminika mitaani na mabarabarani kote nchini humo kushiriki maandamano ya kupinga na kushutumu uchokozi wa kijeshi wa Washington dhidi ya Venezuela, na kutekwa nyara kwa Rais Nicolas Maduro na mkewe, Cilia Flores.

Kuanzia Pwani ya Magharibi hadi Pwani ya Mashariki, waandamanaji wamekusanyika katika kona mbali mbali za Marekani leo Jumapili kuonyesha hasira zao kwa kile walichokitaja kama kitendo cha uchokozi kisicho halali na cha ukiukaji wa sheria, ambacho kinaweza kuitumbukiza tena Marekani katika vita vingine vya muda mrefu.

Huko Seattle, waandamanaji walikusanyika karibu na fukwe za jiji hilo wakipiga nara za, “Watu walioungana hawatashindwa kamwe.” Wengi walibeba mabango yaliyokuwa na jumbe zinazosema uvamizi huo ulikiuka kanuni za kimataifa na sheria za ndani ya nchi.

Huko Philadelphia, mamia waliandamana kutoka ofisi za Baraza la Jiji (City Hall) hadi kituo cha kuandikisha wanajeshi wa Marekani kwenye Mtaa wa Spring Garden, wakipinga vitendo vya Washington dhidi ya Venezuela.

“Congress inahitaji kurudisha mamlaka yake … Wanatakiwa kuwakilisha watu. Sisi ndio tunatakiwa kuamua kama tuende vitani au la,” alisema David Gibson, Mkurugenzi wa vuguvugu la ‘Amani, Haki, Uendelevu SASA!’ na mmoja wa washiriki wa maandamano hayo.

Maandamano ya kulaani ugaidi wa kiserikali wa Marekani dhidi ya Venezuela

Nje ya Ikulu ya Marekani huko Washington, waandamanaji waliimba “Viva, Viva, Venezuela,” huku wakiwa wameshikilia mabango yenye maandishi “No War on Venezuela,” “Komesha Ubeberu wa Marekani,” na “No Blood for Oil.” Waandamanaji wamesema shambulio hilo lilifichua vipaumbele vya kweli vya Washington na nia yake ya kuendelea kutumia nguvu kulazimisha mapenzi yake nje ya nchi.

Huko Illinois, mkusanyiko mkubwa uliofanyika chini ya kaulimbiu “Hakuna Vita dhidi ya Venezuela” uliwavutia washiriki wengi ambao walisema shambulio hilo lilikiuka Katiba ya Marekani, lilihatarisha maisha ya Wamarekani, na lilifikia uingiliaji wa kigeni unaoendeshwa na maslahi ya mafuta badala ya maadili ya kidemokrasia.

Licha ya mvua kubwa, mamia ya watu walikusanyika pia katikati mwa jiji la Los Angeles, wakipaza sauti zao za kulaani operesheni hiyo ya kijeshi dhidi ya Venezuela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *