Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Israel kusitisha mipango yake ya kutoa hukumu za kifo za lazima kwa Wapalestina na kutahadharisha kuwa pendekezo hilo linakiuka sheria za kimataifa.

Volker Turk ametahadharisha kuwa hukumu ya aina hiyo itazidisha“hatari isiyokubalika” ya kuwanyonga watu wasio na hatia.

Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema: “Linapokuja suala la hukumu ya kifo, Umoja wa Mataifa uko wazi kabisa, na unapinga kwa hali zote. Ni vigumu sana kuiambatanisha hukumu hiyo na heshima ya binadamu na inazidisha hatari isiyokubalika ya kuwaua watu wasio na hatia.”

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, mapendekezo hayo hayaendani na wajibu wa Israel kwa mujibu wa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa.

Turk pia ametahadharisha kuwa kuanzisha hukumu za kifo za lazima, ambazo mahakama haina uamuzi wowote mkabala wa hukumu hizo ni kinyume na haki ya kuishi.

Volker Turk amesema kuwa matamshi na lugha zinazotumiwa na wanasiasa wa Israel kuhusu hukumu hizo zinaashiria kuwa hukumu hizo zimekusudiwa kuwalenga Wapalestina tu ambao  mara nyingi hutiwa hatiani baada ya mwenendo wa mashitaka ulio kinyume cha sheria na haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *