Wakazi wa Kata ya Chanika Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma bure za macho kutoka kwa Madaktari Bingwa wa macho kutoka Nchini India, ambapo huduma hizo zitatolewa kwa muda wa siku tatu kuanzia Januari 10 hadi 12,2026 katika Ukumbi wa FDC, katika kata hiyo.

Zoezi hilo litasimamiwa na Ofisi ya Diwani wa Kata ya Chanika, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Handeni Mji, ambapo tayari Madaktari hao wameanza kupokelewa kwaajili ya kutoa fursa ya matibabu bure ya macho, ikiwemo upasuaji wa mtoto wa jicho pamoja na ugawaji wa miwani za aina zote bila malipo.

Zoezi hili linafanyika chini ya ufadhili wa Wadau waliopo chini ya Taasisi ya The Bilal Muslim Mission of Tanzania, likisimamiwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *