Mchambuzi wa masuala ya siasa, Abdulaziz Jaad, amesema kukamatwa kwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, na jeshi la Marekani ni kitendo kinachokiuka sheria za kimataifa.
Jaad amesema operesheni hiyo haikufuata taratibu za kisheria na ilifanyika bila upinzani wowote kutoka kwa viongozi wa kijeshi wa Venezuela, hali inayozua maswali juu ya uhalali wa tukio hilo.
Ameongeza kuwa madai ya rushwa kwa baadhi ya viongozi wa kijeshi yameibuka, yakidaiwa kuchangia kukosekana kwa upinzani wakati wa kukamatwa kwa kiongozi huyo.
✍Ibrahim Kilumbo
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates