Serikali iko katika hatua za mwisho kukamilisha Mfumo wa Kidijitali wa Utoaji wa Taarifa na Maoni kuhusu maafa yanayoweza kutokea, pamoja na namna ya kuyakabili kwa haraka.

Mfumo huo utakuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Idara ya Maafa, na unalenga kuboresha upatikanaji wa taarifa kwa wakati, kuimarisha uratibu na kuchukua hatua za haraka ili kupunguza athari za maafa kwa wananchi na mali zao.

Je, Mfumo huo utasaidia kwa kiasi gani kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa nchini, hasa ikizingatiwa changamoto za upatikanaji wa teknolojia na uelewa wa wananchi?

Tupe maoni yako na yatasomwa kwenye taarifa ya #AdhuhuriLive kuanzia saa 7.00 mchana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *