Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba leo Januari 05, 2026 amefungua Skuli ya Sekondari Chukwani, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Ujenzi wa skuli hiyo umegharimu Sh6.1bilioni ambako lengo ni kuwaandaa vijana wenye maarifa, ujuzi, ubunifu na
maadili, kwa kuunganisha nadharia na vitendo na hivyo kuwa na manufaa mengi ikiwemo kuongeza fursa za elimu bora kwa watoto wa Zanzibar.

Dkt Mwigulu amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika sekta ya elimu.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *