#HABARI: Madereva wa vyombo vya moto katika Manispaa ya Morogoro wameichamkia nishati ya gesi asilia kama mbadala wa mafuta, wakieleza kuwa ni fursa kubwa ya kupunguza gharama za uendeshaji kufuatia kupanda kwa bei ya petroli na dizeli.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha gesi mkoani humo, dereva Leonard Luziro amebainisha kuwa kwa sasa wanatumia kiasi cha shilingi 27,000 tu kununua gesi inayomudu safari ya kwenda hadi mkoani Dodoma.

Mradi huo umezinduliwa rasmi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw. Wazo Mwang’onda, ambaye amesisitiza kuwa matumizi ya nishati safi ni mkakati wa makusudi wa Taifa katika kulinda na kutunza mazingira.

Uongozi wa kiufundi na usimamizi wa kituo hicho, ukiongozwa na Mhandisi Mercy Chilumba pamoja na Salma Salmin, umefafanua kuwa uwekezaji huo una lengo la kuwasaidia wasafirishaji kiuchumi na kuongeza upatikanaji wa nishati hiyo kwa urahisi mkoani hapo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bw. Mussa Kilakala, ameeleza kuwa Mwenge wa Uhuru umekagua, umezindua, na kuweka mawe ya msingi kwenye jumla ya miradi saba ya maendeleo ndani ya manispaa hiyo.

Uzinduzi wa kituo hicho unatajwa na wadau wa usafirishaji kama mapinduzi makubwa yatakayoshusha nauli za abiria na kurahisisha biashara nchini.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA >>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
‎Capitalradio Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *