#HABARI: Serikali imejidhatiti kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kurejesha hadhi ya Mkoa wa Tanga kama kitovu cha viwanda, maarufu kama “Tanga ya Viwanda”.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, wakati wa ziara ya kukagua viwanda vilivyofufuliwa mkoani Tanga. Amesema utekelezaji huo unatokana na agizo la Rais Samia wakati wa ziara yake mkoani humo, ambapo alielekeza viwanda vilivyokufa kufufuliwa ili kuchochea uchumi na ajira.

Waziri Kapinga amesema wizara yake kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Tanga imeanza majadiliano ya kina kwa lengo la kufufua viwanda 18 vya awali, vikiwemo vilivyobinafsishwa pamoja na vile vinavyomilikiwa na watu binafsi.

Ameeleza kuwa kupitia vikao hivyo, Serikali imefanikiwa kubaini changamoto za jumla na changamoto mahususi kwa kila kiwanda, hatua itakayowezesha kuweka mikakati madhubuti ya kurejesha uzalishaji.

Akitolea mfano, Kapinga amesema Kiwanda cha African Hamon, ambacho awali kilikuwa kimesimama kabisa, sasa kimeanza tena uzalishaji na hadi sasa kimeajiri zaidi ya vijana 200 katika ajira za kudumu.

Amesisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha viwanda vyote vilivyolengwa vinafanya kazi kikamilifu ili kuzalisha bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi, hatua itakayosaidia kuitangaza Tanzania kimataifa.

Aidha, Waziri Kapinga amesema Serikali itaweka mtu maalum kwa kila kiwanda ili kurahisisha utatuzi wa changamoto za wawekezaji, kuwapatia kipaumbele katika kushughulikia changamoto zao, kuongeza uzalishaji na kupanua fursa za ajira kwa vijana wa Tanga na taifa kwa ujumla.
Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *