Katibu Mtendaji wa TEITI, Mariam Mgaya, amesema uwekaji wazi wa taarifa za upatikanaji na matumizi ya rasilimali za asili ni hatua muhimu katika kuhakikisha uwajibikaji na manufaa ya rasilimali hizo kwa taifa na wananchi.

Amesema uwazi huo unawezesha wananchi kufahamu mapato yatokanayo na rasilimali kama madini, mafuta na gesi, pamoja na namna fedha hizo zinavyosimamiwa na kutumika katika maendeleo ya nchi.

Kwa mujibu wa Mgaya, fedha zinazopatikana kutokana na rasilimali hizo huingizwa na kuhifadhiwa katika mfuko mkuu wa Serikali, kisha kutumika kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayochochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

✍Ibrahim Kilumbo
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *