Shirikisho la vyombo vya habari vya kimataifa limeikosoa serikali ya Israel kwa kuendelea kutekeleza makataa ya kivizuia vyombo vya Habari kufika kwenye eneo la Gaza, shirikisho hilo likiitaja hatua hiyo kuwa yakusikitisha.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Israel siku ya jumapili  iliiambia Mahakama ya Juu kwamba marufuku hiyo bado itasalia na kutaja hatua hiyo  ni kutokana na  hatari  za kiusalama zinazoendelea  katika eneo la Gaza .

Taarifa hiyo iliwasilishwa kujibu ombi lililowasilishwa na Chama cha Wanahabari wa Kigeni (FPA), ambacho kinawakilisha mamia ya waandishi wa habari wanaofanya kazi nchini Israel na maeneo ya Palestina.

Tangu vita vya Gaza vilipozuka Oktoba 2023, kufuatia shambulio la Hamas, waandishi wa habari wa kigeni wamezuiwa kuingia katika eneo hilo ingawa Wachache tu ndio wameruhusiwa chini ya uagalizi wa  jeshi la Israel.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekuwa akiwahutumu baadhi ya wanahabari kwa kushirikiana na Hamas.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekuwa akiwahutumu baadhi ya wanahabari kwa kushirikiana na Hamas. via REUTERS – Nathan Howard

Chama hicho kiliwasilisha ombi kwa mahakama kwa mara ya kwanza mwaka wa 2024, lakini serikali ya Israel  imekuwa ikiongeza  muda mara kadhaa kabla ya mahakama hiyo  kuweka tarehe 4 Januari kama tarehe ya mwisho ya kusikilizwa kwa ombi hilo.

Mahakama hiyo ya Juu inatarajiwa kutoa uamuzi siku zijazo bila kutaja tarehe rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *