Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya DCEA imekamata kilogamu 9,689.833 za dawa za kulevya, pikipiki kumi na moja, magari matatu pamoja na watuhumiwa 66 wa uhalifu huo.

Akitoa taarifa hiyo leo jijini dar es salaam kamishna jenerali wa DCEA Aretas Lymo amesema Katika operesheni hiyo raia wa Kenya Jefferson Kilonzo aliyetumia biashara ya kuuza chai kuficha biashara ya dawa za kulevya amekamatwa akiwa na gramu 131.88 za heroin.

Nako kwenye mtaa wa Wailes wilayani Temeke pakiti 20 za skanka zenye uzito wa kilogramu 20.03 zikikamatwa ndani ya basi la abiria aina ya Scania la kampuni ya King Masai Tours

Aidha, DCEA inawashikilia Erick Ndagwa, Paul Henry na Tido Mkude waliokamatwa kinyerezi jijini dar es salaam wakiwa na bangi kg 193.66 huku kwa upande mwingine paketi 20 za dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilogramu 9.54 zikikamatwa zikiwa zimefungwa kama majani ya mwarobaini zikisafirishwa kutoka Kenya kuelekea Australia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *