Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dr Samia Suluhu Hassan amezindua Jengo la Taaluma na Utawala Pamoja na Bweni la wanafunzi la Taasisi ya Sayansi Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM-IMS) katika eneo la Buyu, Wilaya ya Mjini Magharibi B, Zanzibar

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali,Rais Samia amesema uwekezaji huo utasaidia kuchochea na kufikia uchumi Jumuishi, huku akisema maarifa yatakayozalishwa chuoni hapo yatasaidia maamuzi ya sera zitakazolinda rasilimali bahari sambamba na kuongeza tija na kipato cha wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *