Wizara ya Katiba na Sheria imesaini makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) pamoja na Legal Services Facility, kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi.

Akizungumza jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi, amesema msaada wa kisheria si hisani bali ni haki ya msingi ya kila Mtanzania, inayotokana na Katiba, utawala bora na wajibu wa Serikali kwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *