Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza mazungumzo ya awali na Wizara ya Kilimo na Wizara ya Maji ili kushirikiana kwenye maeneo ambayo wizara hizo zina muingiliano wa kisekta ili kusaidiana katika kuziinua sekta zote kwa pamoja.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ng’wasi Kamani wakati akizungumza na wafugaji kwenye mnada wa mifugo wa Ndala wilayani Nzega mkoani Tabora.
Mhariri @moseskwindi