Afisa Elimu Sekondari wa Jiji la Dar es Salaam, Mussa Shaban Ally amesema maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza na darasa la kwanza yamekamilika kutokana na ushirikiano wa walimu na viongozi wa serikali.
Amesema watoto wote watapokelewa bila vikwazo na kuanza masomo kwa wakati mmoja.
Aidha meongeza baadhi ya wanafunzi tayari wameripoti na kupewa maelekezo ya awali na kwamba Serikali imeahidi kutatua changamoto za miundombinu ili kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora.
✍Halima Abdallah
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates