Uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa kasi ya kuridhisha ya takribani asilimia 5.9 pungufu kwa asilimia 0.1 ya lengo la asilimia 6 kwa mwaka 2025 huku thamani ya shilingi ikiimarika kwa asilimia 0.8 katika robo ya nne ya mwaka 2025.
Akitoa taarifa ya kamati ya sera ya fedha (MPC), mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Gavana wa Benki Kuu Emmanuel Tutuba, amesema kiwango hicho cha ukuaji wa uchumi na kuimarika kwa shilingi kumetokana na shughuli za kilimo, madini na ujenzi.
Kwa upande wa Zanzibar Gavana Tutuba amesema ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2026 ulifikia asilimia 6.8 ukichangiwa na shughuli za ujenzi, utalii na uzalishaji viwandani.