Walimu na wazazi wa halmashauri ya mji njombe wameiomba serikali kufanya jitihada za haraka kuisaidia shule ya Amali yenye hadhi ya juu inayotaraji kuanza kutoa masomo ya kiuhandisi mwaka huu, ili kuzalisha wataalamu ambao wanaendana na hitaji la kitaifa.
Mombi ya walimu na wazazi yamejikita katika sehemu kuu tatu za muhimu, kwanza ni miundombinu ya ufundishiaji inayoendana na mtaala wa elimu ya amali, pili ni ujenzi wa nyumba za walimu watakao toa ujuzi kwa wanafunzi, na tatu ni upungufu wa walimu watao fundisha masomo ya amali, kwani hadi sasa kuna mwalimu mmoja tu.
Eneo lingine la muhimu ni huduma za kijamii ikiwemo Maji, uzio utakaozunguka shule hiyo pamoja na mkondo wa umeme wa uhakika utakaosaidia wanafunzi kujifunza na kufanya mazoezi kwa vitendo.
Shule hii ya Amali ambayo imejengwa katika kijiji cha Magoda na tayari imekamilika inatarajiwa kuwa mkombozi wa kilio cha ajira kwa vijana wengi nchini.
Hata hivyo huenda hili lisitimie iwapo haitawekewa mazingira yatakayoakisi mahitaji ya jamii inayotaraji kuvuna maarifa hapa.
Mwandishi @dkhan1410
#RFAOnline
#HabariStartv