Mbeya. Serikali mkoani Mbeya,  imeelekeza ununuzi wa bidhaa za huduma  kupitia taasisi za umma kuzingatia misingi ya  uwazi, ,haki ,usawa na ushindani kwa lengo la kulinda ulinzi na maslai ya umma na kuhepuka vitendo vya rushwa.

Hatua hiyo utakuwa  chachu ya kuzingatia sheria za manunuzi umma  kwa kuzingatia Mfumo wa Kieletroniki wa Manunuzi ya Umma (NeST), kwa wazabuni katika kutekeleza miradi mbalimbali ya inayo tangazwa na  Serikali.

Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya, Said Madito amesema jana Januari 10,2026, wakati akifungua mafunzo ya utekelezaji wa sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2023 na kanuni zake za GN namba 518 ya mwaka 2024.

Sheria hizo zimelenga matumizi ya mfumo wa NeST katika ununuzi wa umma kwa wazabuni kutoa mikoa ya  Dar -es- Salaam ,Dodoma ,Mwanza na Mbeya na kuandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

Madito amesema kuwa ili kufikia malengo Serikali itahakikisha mifumo yote ya manunuzi inatoa mazingira wezeshi kwa wazabuni kwa  ushindani wenye uwazi,haki na pasipo upendeleo  kwa kuondoa vikwazo vya mazingira ya rushwa na migogoro .

“Malengo ya mafunzo  ni kuwajengea uwezo wazabuni ,watoa huduma na wakandarasi mbalimbali kujua sheria, kanuni na miongozo ya ununuzi wa umma kupitia mfumo wa NeST,kuanzia  hatua za mchakato wa awali wa manunuzi,”amesema.

Amesema ili kufikia malengi Serikali imekuja na mkakati shiriki kwa kutoa mafunzo kwa makundi hayo ili kuongeza ushindani wa kuomba zabuni za miradi mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kupitia mifumo rasmi.

Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya, Said Madito akifungua mafunzo ya utekelezaji wa sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2023,na kanuni zake za GN namba 518 ya mwaka 2024,ya matumizi ya mfumo wa NeST yaliyo fanyika mkoani hapa.Picha na Hawa Mathias.

“Kupitia fursa hii wazabuni mnaweza kuingia kushindana na makampuni ya ndani na nje na kupata soko la uhakika la bidhaa, lakini ameshangazwa na ushiriki mdogo wa wadau katika mafunzo hayo,”amesema.

Kwa upande wake Kaimu Meneja  PPRA, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Anthony Andason amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wazabuni kuhusiana na sheria za manunuzi ya umma kutumia mifumo ya NeST.

“Mwaka jana tulipanga ratiba ,lakini wazabuni wengi walikuwa na majukumu mengine ya kufunga mwaka na  sasa tumerejesha na kufanyika katika Kanda nne ikiwepo  Nyanda za Juu,”amesema.

Amesema malengo ni kuwapa uelewa wazabuni kwa kuwa wadau wakubwa wa taasisi za Serikali ,lakini cha kushangaza ushiriki umekuwa mdogo tofauti na matarajio kulenga watu 500.

“Tutatoa elimu ya matumizi sahihi ya kutumia mfumo wa NeST ,katika hatua ya taratibu za kuomba zabuni baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto  ya uwelewa wa kushiriki zabuni za umma kupitia mfumo rasmi huo, “amesema.

Naye Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi wa barabara,Hussen Mwakalobo amesema mfumo huo utawasaidia kupata zabuni za miradi tofauti na miaka ya nyuma .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *