Mabao mawili yaliyoipa ushindi timu ya Taifa ya Argentina dhidi ya Austria ni zawadi ya kuzaliwa ya Lionel Messi anayetimiza umri wa miaka 39 keshokutwa Jumatano.

Nahodha na nguli wa soka wa Argentina, Lionel Messi, ameendelea kuwasha moto kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2026, baada ya kuandika mabao mawili akiwa ametimiza mabao 18 kwenye mashindano hayo makubwa duniani.

Kwenye mchezo na Austria baadhi ya mashabiki walikuwa na mabango yaliyokuwa yakimtakia Messi heri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa yakiandikwa “Happy Birthday.”

Mbali na bango la kumtakia kheri ya kuzaliwa Messi, pia kulikuwa na bango lililoonyeshwa na shabiki bibi mzee wa Argentina likiwa na maandishi “ni shabiki wa Messi mwenye umri wa miaka 100”.

Bango lililoonyeshwa na shabiki bibi mzee wa Argentina likiwa na maandishi “ni shabiki wa Messi mwenye umri wa miaka 100”.

Katika mchezo wa jana Jumatatu Juni 23, 2026, Argentina imeichapa Austria mabao 2-0, yote yamefungwa na Messi ikiwa ni ishara ya kujitakia ‘Happy Birthday’ ya umri mpya wa miaka 39 unaotimia kesho, Jumatano ya Juni 24, 2026.

Alizaliwa Juni 24, 1987 katika Hospitali ya Italiano Garibaldi iliyopo Rosario, Argentina.

Alizaliwa kwenye familia ya hali ya chini, babu yake akiwa Jorge Horacio Messi aliyekuwa mfanyakazi wa kiwanda cha chuma.

Rosario, mji wa bandari uliopo pembezoni mwa Mto Paraná unajulikana kihistoria kama chimbuko la vipaji vikubwa vya soka na viwanda Argentina.

Nahodha wa Argentina, Lionel Messi akishangilia bao la pili katika mechi ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Austria. Picha na Mtandao

Messi alikulia katika mtaa maskini wa Las Heras uliopo kusini mwa Rosario, ambako alianza kucheza soka la mtaani na kaka zake, Rodrigo na Matías, pamoja na binamu zake, Emmanuel na Maxi Biancucchi.

Akiwa na umri wa miaka minne tu, alijiunga na klabu ya mtaani ya Grandoli iliyokuwa ikifundishwa na baba yake.

Baadaye akiwa na umri wa miaka sita (1994), alihamia klabu kubwa ya jiji hilo, Newell’s Old Boys, ambako alifunga mabao karibu 500 kwenye kikosi cha watoto kilichopewa jina la “The Machine of ’87

Imeandikwa na Noor Shija kwa msaada wa mtandao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *