Dar es Salaam. Mshindi wa gari aina ya Subaru XT Forester, Magdalena Nkuba, amekabidhia gari hilo huku akisema kuwa kwake ni kama amezaliwa upya.
Nkuba kutoka mkoani Simuyu, amekabidhiwa gari hilo na Kampuni ya Mawasiliano ya Haloteli, leo Jumatatu Januari 13, 2026, baada ya kuibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa wiki iliyipota.
Droo hiyo inatokana na kampeni ya Halotel kutimiza miaka 10 ya utoaji wa huduma za mawasiliano hapa nchini.
Nkuba ambaye ni mkulima na mama wa watoto kadhaa, alitangazwa kuwa mshindi wa gari hilo Januari 6, 2026 katika droo kubwa iliyochezeshwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jijini Dar es salaam baada ya kukabidhiwa gari hilo rangi nyeupe, Nkuba amesema gari hilo kwake limempa furaha kama mtu aliyezaliwa upya.
Nkumba amesema haikuwa rahisi na hata alivyopigiwa simu ya kupewa taarifa kuwa ameshinda gari, hakuamini.
“Siku niliyopigiwa simu kuwa nimeshinda gari, sikuamini niliona kama wananichelewesha kwa sababu nilikuwa shambani, hivyo niliendelea kulima siku pokea simu na ilivyopigwa kwa mara ya pili ndio nikaipokea sasa,” amesema Magdalena na kuongeza
“Nilipopokea simu ile kwa mzaha mzaha tu, yaani sikuamini walivyosema Magdalena umeshinda gari aina ya Subaru, kwa kweli bado sikuamini, lakini leo nimeamini baada ya kukabidhiwa hapa” amesema Magdalena.
Amesema gari hiyo ataliendesha mwenyewe na wala hata uza wala kumpa mtu.
“Nimefurahi sana kushinda gari, najua halotel inawezesha na ninaomba wenzangu wanaotumia Halotel waendelee kutumia huduma hiyo ili nao waweze kujishindia gari” amesema ba kuongeza
Magdalena amesema mwaka 2026 umekuwa ni mwaka mzuri kwake kwa kupata gari ambayo ataitumia yeye na familia yake katika kazi zake za kila siku.
“Halotel wamefanikisha mimi na familia yangu kuwa na maisha mapya baada ya kupata gari,” amesema
Shabani Seif ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja kutoka kampuni ya Halotel, Nkuba amejipatia gari hilo baada ya vuna pointi kupitia miamala na vocha.
Seif amesema kampuni yake imejipanga mwaka huu kuwapatia zawadi kubwa wateja wake.
Alisema Oktoba 2025 walianzisha kampeni ya kufikisha miaka 10 ya utoaji wa huduma za mawasiliano hapa nchini na kampeni hii iliendeshwa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Oktoba.
Katika promosheni hiyo, mbali na kutoa gari pia walichezesha droo na kupata washindi wa fedha taslimu Sh2 milioni.
Hata hivyo, ndani ya kipindi hicho cha miaka 10 tangu ianze kutoa huduma za mawasiliano kampuni hiyo imefikisha wateja 16.5 milioni nchi nzima.
Idadi hiyo ya wateja ni kuanzia mwaka 2015 ilipoanzishwa kampuni hiyo hapa nchini hadi Septemba 2025.
